Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya sh milioni moja kwa Peter Celestine, mmoja wa washindi wa shindano la kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali wakati wa shindano hilo jijini Dar es Salaam jana. Shindano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Tanzania Youth Alliance (Tayoa) kwa udhamini wa benki za NBC na Barclays. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika na Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC Tanzania, Mussa Jallow.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya sh milioni moja kwa Frank Mauggo, mmoja wa washindi wa shindano la kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali wakati wa shindano hilo jijini Dar es Salaam jana. Shindano hilo linafanyika kwa udhamini wa benki za NBC na Barclays. Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika.
Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika (kushoto) akizungumza muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) kuzindua shindano la kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana liitwalo ‘Vijanatz Business Plan competition’ chini ya udhamini wa benki za NBC na Barclays.
Burudani ya kucheza na nyoka ilipamba sherehe za uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (kulia), akipozi kwa picha na nyoka wa wacheza ngoma katika hafla hiyo.
Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiwa kazini wakati baadhi ya washiriki wakitoa mada zao.
Picha ya kumbukumbu; Ujumbe wa benki ya NBC, na Barclays Afrika, washiriki wa shindano la Vijanatz Business Plan na viongozi wa Tayoa wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.