Wanaume mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha dhana potofu kuwa tohara inapunguza nguzu za kiume na maumbile ya viungo vyao vya uzazi na badala yake wajitokeze kwa wingi kupata huduma hiyo bure katika zahanati na vituo vya afya ili kuwakinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Emmily Mushi afisa tathimini kutoka Shirika lisilo la kiserikali la (TAYOA) kwenye semina juu ya kampeni ya Tohara+ iliyowajumuisha madiwani kutoka Halmashauri za Ushetu, Msalala na Mji wa kahama ambazo zote za mkoa wa shinyanga.
Amesema baadhi wanaume mkoani humo ambao hawajafanyiwa tohara wanaogopa kufanyiwa tohara kwa kudhani itapunguza nguvu za kiume jambo halina ukweli wowote na badalayake wajitokeze kwa wingi katika kampeni hiyo ambayo inatolewa bure na (TAYOA) kwa kushirikiana na Madaktari bigwa.
Amefafanua kuwa katika kampeni hiyo TAYOA imekusudia kuwafikia vijana elfu 7000 wenye umri wa miaka 17 hadi 25 katika mkoa wa Shinyanga hivyo ni budi wakajitokeza kupata huduma hiyo ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kundi hilo ambao hawafanyiwa Tohara.
Naye diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto Tabu ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu amesema watu wazima wemeshindwa kushiriki katika kampeni ya Tohara kwa kuona aibu na wengine wakiihusisha na mtandao wa freemason na kuiomba jamii kuachana na dhana hiyo potofu.
Amewataka watu wazima kutoona aibu na badala yake wafike katika vituo vya afya kupata huduma hiyo bure ambayo serikali inatumia gharama kubwa kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Igwamanoni HAMIDU MRISHO amesema ni vyema TAYOA ikatenga maeneo maalumu kwaajili ya wanaume wenye umri mkubwa katika kuwapatia Tohara ikiwemo kupewa kipaumbele pindi wanapofika kupata huduma hiyo.
Kampeni ya Tohara+ bure kwa wanaume inatekelezwa bure na TAYOA katika mikoa 7 hapa nchini na katika mkoa wa shinyanga inalenga kuwafikia watu 7000.