Waziri Gwajima aipongeza Tayoa kwa kushirikiana na serikali

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, amepongeza ushirikiano wa Shirika la Vijana (Tayoa) kwa serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Ameyasema hayo leo Septemba 16, 2021 jijini Dodoma alipotembelea banda la Shirika hilo na kuelezwa kazi zinazofanywa ns shirika hilo ikiwemo kusambaza kondom na makasha ya kusambazia mipira hiyo vijijini.

Maonyesho hayo yamefanyika pembeni ya mkutano mkuu wa mwaka uliowashirikisha waganda wakuu wa mikoa yote nchini na wa halmashauri na kufanyika kweye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Gwajima amesema huduma ya usambazaji mipira ya kiume ni muhimu sana hivyo shirika hilo ni vyema likaendelea kusambaza ili kuwafikia vijana wengi nchini hali ambayo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na ugonjwa huo hatari.

“Nawashukuru sana Tayoa mmekuwa mkishirikiana vyema na serikali na endeleeni kuhakikisha huduma zenu za kusambaza mipira ya kiume zinawafikia watu wengi zaidi,” alisema Waziri Gwajima

Akizungumza kwenye mkutano huo, Waziri Gwajima amefurahishwa na kauli mbiu ya mkutano huo inayosema ustahimilivu wa mifumo ya afya katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

Amesema pamoja na changamoto zilizopo waganda wakuu wa mikoa na halmashauri wameendelea kutumia weledi wao kutumikia jamii katika mapambano ya ugonjwa huo.

“Hili ni jambo la kizalendo hongereni na nichukue nafasi hii kuwaelekeza viongozi wote kuhamasisha wananchi kwenda kupata chanjo ya COVID 19 kwani chanjo hiyo ni salama” alisema Dk. Doroth Gwajima

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akionyesha kondom aina ya safari inayosambazwa na Shirika la Vijana Nchini (Tayoa) kwenye maonyesho yaliyofanyika pembeni ya mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa, Peter Masika kuhusu makasha ya kusambazia kondom na kondom aina ya safari zinazosambazwa na shirika hilo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akibonyeza mashine kwaajili ya kutoa kondom aina ya safari inayosambazwa na shirika la vijana nchini Tayoa wakati wa maonyesho yaliyofanyika pembeni ya mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa Peter Masika akimweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima kuhusu makasha ya kusambazia kondom kwenye maonyesho yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Leave A Comment

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Choose Demos Submit a Ticket Purchase Theme

Pre-Built Demos Collection

Consultio comes with a beautiful collection of modern, easily importable, and highly customizable demo layouts. Any of which can be installed via one click.

Cryptocurrency
Business Construction
Business Coach
Consulting
Immigration
Finance 2
Corporate 1
Corporate 2
Corporate 3
Consulting
Business 1
Business 2
Business 3
IT Solution
Tax Consulting
Human Resource
Life Coach
Marketing
Insurance
Finance RTL
Marketing
Consulting
Consulting